1 Samuel 20:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, Shauli hakusema lolote, kwani alifikiri kuwa labda Daudi amepatwa na tatizo au yeye si safi kuhudhuria sherehe hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamu; hakika yeye yu najisi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Sauli hakusema neno siku ile; maana alidhani ya kuwa, Amepatikana na neno, hakutakata; hakosi yeye hakutakata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, Shauli hakusema lolote, kwani alifikiri kuwa labda Daudi amepatwa na tatizo au yeye si safi kuhudhuria sherehe hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli hakusema cho chote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Sauli hakusema neno siku ile; maana alidhani ya kuwa, Amepatikana na neno, hakutakata; hakika yeye hakutakata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, Shauli hakusema lolote, kwani alifikiri kuwa labda Daudi amepatwa na tatizo au yeye si safi kuhudhuria sherehe hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini siku hiyo Sauli hakusema neno, kwani alisema moyoni: Labda liko tukio lililompata, asiwe ametakata, kwa kuwa hakueuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Sauli hakusema neno siku ile; maana alidhani ya kuwa, Amepatikana na neno, hakutakata; hakosi yeye hakutakata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, Saulo hakusema neno lolote, maana alifikiri kwamba labda Daudi amepatwa na tatizo au yeye si safi kwa kuhuzuria sikukuu hiyo.