1 Samuel 20:34 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yonathani, huku akiwa amekasirika sana, aliondoka mezani kwa haraka, wala hakula chakula chochote siku hiyo ya pili ya sherehe za mwezi mwandamo. Yonathani alihuzunika sana juu ya Daudi kwa sababu baba yake alikuwa amemwaibisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yonathani akainuka kutoka mezani kwa hasira kali. Siku ile ya pili ya mwezi hakula chakula, kwa kuwa alikuwa amehuzunishwa na vitendo vya aibu ambavyo baba yake alikuwa anamtendea Daudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yonathani akaondoka pale mezani, mwenye hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yonathani, huku akiwa amekasirika sana, aliondoka mezani kwa haraka, wala hakula chakula chochote siku hiyo ya pili ya sherehe za mwezi mwandamo. Yonathani alihuzunika sana juu ya Daudi kwa sababu baba yake alikuwa amemwaibisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yonathani akainuka kutoka mezani kwa hasira kali. Siku ile ya pili ya mwezi hakula chakula, kwa kuwa alikuwa amehuzunishwa na vitendo vya aibu baba yake alivyokuwa anamtendea Daudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yonathani akainuka kutoka mezani kwa hasira kali. Siku ile ya pili ya mwezi hakula chakula, kwa kuwa alikuwa amehuzunishwa na vitendo vya aibu ambavyo baba yake alikuwa anamtendea Daudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yonathani akaondoka pale mezani, akiwa na hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yonathani, huku akiwa amekasirika sana, aliondoka mezani kwa haraka, wala hakula chakula chochote siku hiyo ya pili ya sherehe za mwezi mwandamo. Yonathani alihuzunika sana juu ya Daudi kwa sababu baba yake alikuwa amemwaibisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yonatani akaondoka hapo mezani kwa makali yaliyowaka moto, hakula chakula cho chote siku hiyo ya pili ya mwandamo wa mwezi, kwani alimsikitikia Dawidi, kwa kuwa baba yake amemtukana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yonathani akaondoka pale mezani, mwenye hasira kali, wala hakula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi sana, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yonatani, akiwa amekasirika sana, aliondoka kwenye meza kwa haraka, wala hakukula chakula chochote siku hiyo ya pili ya sikukuu ya mwandamo mwezi. Yonatani alihuzunika sana juu ya Daudi kwa sababu baba yake alikuwa amemupatisha haya.