1 Samuel 20:41 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara yule kijana alipokwisha ondoka, Daudi akainuka na kutoka mahali alipojificha karibu na rundo la mawe. Aliinama chini kwa heshima mara tatu mbele ya Yonathani. Wote wawili, Daudi na Yonathani, wakakumbatiana na kulia. Daudi alikuwa na uchungu zaidi kuliko Yonathani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara yule kijana alipokwisha ondoka, Daudi akainuka na kutoka mahali alipojificha karibu na rundo la mawe. Aliinama chini kwa heshima mara tatu mbele ya Yonathani. Wote wawili, Daudi na Yonathani, wakakumbatiana na kulia. Daudi alikuwa na uchungu zaidi kuliko Yonathani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara yule kijana alipokwisha ondoka, Daudi akainuka na kutoka mahali alipojificha karibu na rundo la mawe. Aliinama chini kwa heshima mara tatu mbele ya Yonathani. Wote wawili, Daudi na Yonathani, wakakumbatiana na kulia. Daudi alikuwa na uchungu zaidi kuliko Yonathani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtoto alipokwisha kwenda, Dawidi akatokea upande wa kusini, akauinamisha uso wake chini mara tatu na kumwangukia mara tatu, kisha wakanoneana na kulia machozi pamoja wao wawili, lakini Dawidi akazidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule kijana alipokwisha kuondoka, Daudi akasimama na kutoka pahali alipojificha karibu na lundo la mawe. Aliinama chini kwa heshima mara tatu mbele ya Yonatani. Wote wawili, Daudi na Yonatani, wakakumbatiana na kulia. Daudi alikuwa na uchungu zaidi kuliko Yonatani.