1 Samuel 20:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwambia, “Kesho ni sherehe za mwezi mwandamo, nami natazamiwa kuwapo mezani kula pamoja na mfalme. Lakini niache, nikajifiche huko shambani hadi siku ya tatu jioni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Daudi akamwambia Yonathani, “Angalia, kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo, nami inanipasa kula chakula pamoja na mfalme; lakini niache niende kujificha shambani hadi kesho kutwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwambia, “Kesho ni sherehe za mwezi mwandamo, nami natazamiwa kuwapo mezani kula pamoja na mfalme. Lakini niache, nikajifiche huko shambani hadi siku ya tatu jioni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Daudi akasema, “Angalia, kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo, nami inanipasa kula chakula pamoja na mfalme, lakini niache niende kujificha shambani mpaka kesho kutwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Daudi akamwambia, “Angalia, kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo, nami inanipasa kula chakula pamoja na mfalme; lakini niache niende kujificha shambani mpaka kesho kutwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hadi siku ya tatu jioni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwambia, “Kesho ni sherehe za mwezi mwandamo, nami natazamiwa kuwapo mezani kula pamoja na mfalme. Lakini niache, nikajifiche huko shambani hadi siku ya tatu jioni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwambia Yonatani: Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi; hapo inanipasa kula mezani pa mfalme, lakini nipe ruhusa, nijifiche shambani hata siku ya tatu jioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hata siku ya tatu jioni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia: “Kesho ni sikukuu ya mwandamo wa mwezi, nami nilipaswa kuwa kwenye meza kwa kula pamoja na mufalme. Lakini uniache, niende kujificha kule katika shamba mpaka siku ya tatu magaribi.