1 Samuel 21:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watumishi wa mfalme wakamwambia Akishi, “Huyu si Daudi, mfalme wa nchi ya Israeli? Je, si huyu ambaye walikuwa wakiimbiana juu yake katika ngoma, wakisema, ‘Shauli ameua maelfu yake na Daudi ameua makumi elfu yake?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema: “ ‘Sauli amewaua elfu zake, naye Daudi makumi elfu yake’?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watumishi wa mfalme wakamwambia Akishi, “Huyu si Daudi, mfalme wa nchi ya Israeli? Je, si huyu ambaye walikuwa wakiimbiana juu yake katika ngoma, wakisema, ‘Shauli ameua maelfu yake na Daudi ameua makumi elfu yake?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema: “ ‘Sauli amewaua elfu zake, naye Daudi makumi elfu yake’?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, “Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema: “ ‘Sauli amewaua elfu zake, naye Daudi makumi elfu yake’?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watumishi wa mfalme wakamwambia Akishi, “Huyu si Daudi, mfalme wa nchi ya Israeli? Je, si huyu ambaye walikuwa wakiimbiana juu yake katika ngoma, wakisema, ‘Shauli ameua maelfu yake na Daudi ameua makumi elfu yake?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watumishi wa Akisi wakamwambia: Kumbe huyu siye Dawidi, mfalme wa nchi ile? Siye yeye, waliyemwimbia na kuitikiana na kumchezea kwamba: Sauli ameua elfu lake, lakini Dawidi ameua maelfu yake kumi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, Daudi alimukimbia Saulo, akaenda kwa mufalme Akisi wa Gati.