1 Samuel 21:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, akabadilisha tabia yake, akijifanya mwendawazimu, akawa anakwaruzakwaruza kwenye malango ya mji, na mate yake akayaacha yatiririke kwenye ndevu zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango, na kuachia mate kutiririka kwenye ndevu zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, akabadilisha tabia yake, akijifanya mwendawazimu, akawa anakwaruzakwaruza kwenye malango ya mji, na mate yake akayaacha yatiririke kwenye ndevu zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi akajifanya mwenda wazimu mbele yao, naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakunakuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, akabadilisha tabia yake, akijifanya mwendawazimu, akawa anakwaruzakwaruza kwenye malango ya mji, na mate yake akayaacha yatiririke kwenye ndevu zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo akayageuza mawazo yake mbele yao, akawa kama mwenye wazimu huko kwao, akaipiga milango ya lango la mji kama ngoma, nayo mate yake akayachuruzisha madevuni mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakuna-kuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akafikiri sana juu ya maneno yale, akaanza kumwogopa sana Akisi mufalme wa Gati.