1 Samuel 21:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo kuhani Ahimeleki akampa mikate mitakatifu, kwani hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya kuwekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ikabadilishwa na mikate mipya kutoka mekoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonesho, iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za Mwenyezi Mungu na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya Wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za Bwana, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo kuhani Ahimeleki akampa mikate mitakatifu, kwani hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya kuwekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ikabadilishwa na mikate mipya kutoka mekoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwepo mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonyesho iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za BWANA na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo kuhani akampa ile mikate iliyowekwa wakfu, kwa kuwa hapakuwepo mikate mingine isipokuwa hiyo ya Wonyesho iliyokuwa imeondolewa hapo mbele za bwana na kubadilishwa na mingine yenye moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za BWANA, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo kuhani Ahimeleki akampa mikate mitakatifu, kwani hapakuwa na mikate mingine isipokuwa hiyo ya kuwekwa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ikabadilishwa na mikate mipya kutoka mekoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji alipompa ile mikate mitakatifu, kwani haikuwako mikate mingine, isipokuwa ile mikate, aliyowekewa Bwana, nayo huondolewa machoni pa Bwana, wakiweka hapo mikate mingine yenye moto; ni siku ileile, hiyo ya mbele inapochukuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya Wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za BWANA, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia: “Kwa hakika, ninapokwenda kwa ajili ya shuguli kubwa, wanawake wanatengwa mbali nasi! Ikiwa miili ya vijana wangu inakuwa mitakatifu na safi tunapokuwa kwenye shuguli za kawaida, basi, si zaidi katika shuguli hii kubwa?”