1 Samuel 21:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi kulikuwa hapo siku hiyo mtumishi mmoja wa Shauli ambaye alikuwa amezuiliwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mtumishi huyo aliitwa Doegi, Mwedomu, msimamizi wa wachungaji wa Shauli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi siku hiyo palikuwepo mmoja wa watumishi wa Sauli, aliyezuiliwa mbele za Mwenyezi Mungu; alikuwa Doegi Mwedomu, kiongozi wa wachungaji wa Sauli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za Bwana jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi kulikuwa hapo siku hiyo mtumishi mmoja wa Shauli ambaye alikuwa amezuiliwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mtumishi huyo aliitwa Doegi, Mwedomu, msimamizi wa wachungaji wa Shauli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi siku hiyo palikuwepo na mmoja wa watumishi wa Sauli, aliyezuiliwa mbele za BWANA, jina lake Doegi, Mwedomu, kiongozi wa wachunga wanyama wa Sauli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi siku hiyo palikuwepo na mmoja wa watumishi wa Sauli, aliyezuiliwa mbele za bwana; alikuwa Doegi Mwedomu, kiongozi wa wachunga wanyama wa Sauli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za BWANA jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi kulikuwa hapo siku hiyo mtumishi mmoja wa Shauli ambaye alikuwa amezuiliwa mbele ya Mwenyezi-Mungu. Mtumishi huyo aliitwa Doegi, Mwedomu, msimamizi wa wachungaji wa Shauli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile kukawako mmoja wao watumishi wa Sauli, naye alikuwa ametengwa, akae machoni pa Bwana, jina lake Doegi wa Edomu aliyekuwa mkuu wa wachungaji wa Sauli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za BWANA jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo kuhani Ahimeleki akamupa mikate mitakatifu, maana hapakukuwa mikate mingine isipokuwa ile ambayo inaondolewa mbele ya Yawe na kubadilishwa na mikate mipya kutoka kwenye jiko.