1 Samuel 22:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli akamwambia, “Kwa nini wewe na Daudi mwana wa Yese, mmekula njama dhidi yangu? Kwa nini ulimpatia mikate na upanga, halafu ukamwombea kwa Mungu? Kwa sababu hiyo, leo ameniasi na ananivizia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga njama dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena, ulimuuliza Mungu kwa ajili yake na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniondokee na kunivizia kama hivi leo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli akamwambia, “Kwa nini wewe na Daudi mwana wa Yese, mmekula njama dhidi yangu? Kwa nini ulimpatia mikate na upanga, halafu ukamwombea kwa Mungu? Kwa sababu hiyo, leo ameniasi na ananivizia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga tena kumwuliza Mungu kwa ajili yake, kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena hukumuuliza Mungu kwa ajili yake, na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniasi na kunivizia kama hivi leo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli akamwambia, “Kwa nini wewe na Daudi mwana wa Yese, mmekula njama dhidi yangu? Kwa nini ulimpatia mikate na upanga, halafu ukamwombea kwa Mungu? Kwa sababu hiyo, leo ameniasi na ananivizia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akamwuliza: Mbona mmenivunjia maagano, wewe na mwana wa Isai? Nawe umempa chakula na upanga, ukamwuliza Mungu kwa ajili yake, apate kuniinukia na kuniotea kama yanavyoelekea leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauli akamwuliza, Mbona mmefanya fitina juu yangu, wewe na mwana wa Yese? Kwa maana umempa mikate, na upanga, nawe umemwuliza Mungu kwa ajili yake, ili aniondokee na kunivizia kama hivi leo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo akamwambia: “Kwa nini wewe na Daudi mwana wa Yese, mumenifanyia shauri baya? Kwa nini ulimupatia mikate na upanga, halafu ukamwombea kwa Mungu? Kwa sababu hiyo, leo ameniasi na ananivizia.”