1 Samuel 22:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli akawaambia walinzi waliokuwa wamesimama kandokando yake, “Geukeni na kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu, maana wao wanapatana na Daudi; walijua kuwa ametukimbia wala hawakuniarifu.” Lakini walinzi hao hawakuinua mikono yao ili kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Mwenyezi Mungu, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.” Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa Bwana, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli akawaambia walinzi waliokuwa wamesimama kandokando yake, “Geukeni na kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu, maana wao wanapatana na Daudi; walijua kuwa ametukimbia wala hawakuniarifu.” Lakini walinzi hao hawakuinua mikono yao ili kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake akisema, “Geukeni na kuwaua makuhani wa BWANA, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.” Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa bwana, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.” Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa BWANA, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli akawaambia walinzi waliokuwa wamesimama kandokando yake, “Geukeni na kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu, maana wao wanapatana na Daudi; walijua kuwa ametukimbia wala hawakuniarifu.” Lakini walinzi hao hawakuinua mikono yao ili kuwaua makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme akawaagiza wapiga mbio waliosimama hapo na kumzunguka: Wageukieni hawa watambikaji wa Bwana, mwaue! Kwani mikono yao nayo humsaidia Dawidi, tena walijua, ya kuwa anakimbia, lakini hawakuyafunua masikioni pangu. Lakini watumishi wa mfalme wakakataa kuinyosha mikono yao kuwakumba watambikaji wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mfalme akawaambia askari walinzi waliosimama karibu naye Geukeni, mkawaue hao makuhani wa BWANA, kwa sababu mkono wao u pamoja na Daudi, na kwa sababu walijua ya kuwa amekimbia, wasiniarifu. Lakini watumishi wa mfalme walikataa kunyosha mkono na kuwaangukia makuhani wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo akawaambia walinzi waliokuwa wakisimama pembeni yake: “Mugeuke na kuwaua makuhani wa Yawe, maana wao wanapatana na Daudi; walijua kwamba ametukimbia wala hawakuniarifu.” Lakini walinzi hao hawakuinua mikono yao kwa kuwaua makuhani wa Yawe.