1 Samuel 22:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, mfalme Shauli akamwambia Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Doegi, Mwedomu, akaenda na kuwaua makuhani wote. Siku hiyo, Doegi aliua makuhani themanini na watano ambao huvaa vizibao vya kikuhani vya kitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mfalme akamwagiza Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano waliovaa vizibau vya kitani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, ukawaangukia hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, mfalme Shauli akamwambia Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Doegi, Mwedomu, akaenda na kuwaua makuhani wote. Siku hiyo, Doegi aliua makuhani themanini na watano ambao huvaa vizibao vya kikuhani vya kitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mfalme akamwagiza Doegi, akisema, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi, Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano wavaao visibau vya kitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mfalme akamwagiza Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano wavaao visibau vya kitani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, uwaangukie hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, mfalme Shauli akamwambia Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Doegi, Mwedomu, akaenda na kuwaua makuhani wote. Siku hiyo, Doegi aliua makuhani themanini na watano ambao huvaa vizibao vya kikuhani vya kitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme alipomwambia Doegi. Waangukie wewe, uwakumbe hawa watambikaji! Basi, Doegi wa Edomu akawaangukia, akawakumba hawa watambikaji, akawaua siku hiyo watu 85 waliovaa visibau vya mtambikaji vya ukonge.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme akamwambia Doegi, Geuka wewe, ukawaangukia hao makuhani. Basi Doegi, Mwedomi, akageuka, akawaangukia makuhani, akaua siku ile watu themanini na watano wenye kuvaa naivera ya kitani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, mufalme Saulo akamwambia Doegi: “Wewe geuka uwaue makuhani.” Doegi Mwedomu akaenda na kuwaua makuhani wote. Siku hiyo, Doegi aliua makuhani makumi nane na watano ambao wanavaa vizibao vya kikuhani vya kitani.