1 Samuel 22:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Shauli akawaambia watumishi wake, “Sasa nyinyi watu wa kabila la Benyamini nisikilizeni, je, mnadhani huyu Daudi mwana wa Yese atampa kila mmoja wenu mashamba na mashamba ya mizabibu? Au je, mnadhani atamfamya kila mmoja wenu kamanda wa maelfu au kamanda wa mamia ya majeshi?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi Wabenyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa maakida wa watu elfu, na maakida wa watu mia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Shauli akawaambia watumishi wake, “Sasa nyinyi watu wa kabila la Benyamini nisikilizeni, je, mnadhani huyu Daudi mwana wa Yese atampa kila mmoja wenu mashamba na mashamba ya mizabibu? Au je, mnadhani atamfamya kila mmoja wenu kamanda wa maelfu au kamanda wa mamia ya majeshi?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa wakuu wa watu maelfu, na wakuu wa watu mamia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Shauli akawaambia watumishi wake, “Sasa nyinyi watu wa kabila la Benyamini nisikilizeni, je, mnadhani huyu Daudi mwana wa Yese atampa kila mmoja wenu mashamba na mashamba ya mizabibu? Au je, mnadhani atamfamya kila mmoja wenu kamanda wa maelfu au kamanda wa mamia ya majeshi?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Sauli alipowaambia watumishi wake waliosimama na kumzunguka: Sikilizeni, ninyi Wabenyamini! Mwana wa Isai atawezaje kuwapa ninyi nyote mashamba na mizabibu? Tena atawezaje kuwaweka ninyi nyote kuwa wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa maakida wa watu elfu, na maakida wa watu mia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Saulo akawaambia watumishi wake: “Sasa ninyi watu wa kabila la Benjamina munisikilize, munazani kwamba huyu Daudi mwana wa Yese atamupa kila mumoja wenu mashamba ya mizabibu na mashamba mengine? Au munazani kwamba atamufanya kila mumoja wenu kuwa mukubwa wa waaskari maelfu au mukubwa wa waaskari mamia?