1 Samuel 23:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Daudi akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa hakika mimi mtumishi wako, nimesikia kwamba Shauli anapanga kuja kuangamiza mji wa Keila kwa sababu yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akasema, “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mtumishi wako amesikia kwa hakika kwamba Sauli anapanga kuja Keila na kuangamiza mji kwa ajili yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Daudi akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa hakika mimi mtumishi wako, nimesikia kwamba Shauli anapanga kuja kuangamiza mji wa Keila kwa sababu yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akasema, “Ee BWANA, Mungu wa Israeli, mtumishi wako amesikia kwa hakika kwamba Sauli anapanga kuja Keila na kuangamiza mji kwa ajili yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akasema, “Ee bwana, Mungu wa Israeli, mtumishi wako amesikia kwa hakika kwamba Sauli anapanga kuja Keila na kuangamiza mji kwa ajili yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, mimi mtumishi wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Daudi akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa hakika mimi mtumishi wako, nimesikia kwamba Shauli anapanga kuja kuangamiza mji wa Keila kwa sababu yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akaomba: Bwana Mungu wa Isiraeli, msikilize vema mtumishi wako! Kwani Sauli anatafuta njia ya kuingia Keila, auangamize mji huu kwa ajili yangu mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Daudi akaomba: “Ee Yawe, Mungu wa Israeli, kwa hakika mimi mutumishi wako, nimesikia kwamba Saulo anapanga kuja kuangamiza muji wa Keila kwa sababu yangu.