1 Samuel 23:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.” Naye Mwenyezi Mungu akasema, “Ndiyo, atashuka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye Bwana akamjibu, Atashuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atatelemka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee BWANA, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.” Naye BWANA akasema, “Ndiyo, atashuka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, watu wa Keila watanisalimisha kwake? Je, Sauli atateremka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee bwana, Mungu wa Israeli, mwambie mtumishi wako.” Naye bwana akasema, “Ndiyo, atashuka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumishi wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumishi wako. Naye BWANA akamjibu, Atashuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Je, wakazi wa Keila watanitia mikononi mwa Shauli? Je, Shauli atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mtumishi wako? Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nakuomba unijibu mimi mtumishi wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Shauli atakuja.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa je? Wenyeji wa Keila watanitoa na kunitia mkononi mwake Sauli, atakaposhuka, kama mtumishi wako alivyosikia? Bwana Mungu wa Isiraeli, hili mwambie mtumishi wako! Bwana akasema: Atashuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye BWANA akamjibu, Atashuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wa Keila watanitia katika mikono ya Saulo? Saulo atakuja kweli kama nilivyosikia mimi mutumishi wako? Ee Yawe, Mungu wa Israeli, ninakuomba unijibu mimi mutumishi wako.” Yawe akamujibu: “Saulo atakuja.”