1 Samuel 23:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yonathani alimwambia, “Usiogope, baba yangu Shauli hatakupata. Wewe utakuwa mfalme wa Israeli, mimi nitakuwa wa pili wako. Hata Shauli baba yangu anajua jambo hili.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Usiogope, Daudi; baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa wa pili wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yonathani alimwambia, “Usiogope, baba yangu Shauli hatakupata. Wewe utakuwa mfalme wa Israeli, mimi nitakuwa wa pili wako. Hata Shauli baba yangu anajua jambo hili.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Usiogope, Daudi; baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Usiogope, Daudi; baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa makamu wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yonathani alimwambia, “Usiogope, baba yangu Shauli hatakupata. Wewe utakuwa mfalme wa Israeli, mimi nitakuwa wa pili wako. Hata Shauli baba yangu anajua jambo hili.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwambia: Usiogope! Kwani mkono wa baba yangu Sauli hautakupata, ila wewe utakuwa mfalme wao Waisiraeli, nami nitakuwa wa pili akufuataye; hata baba yangu Sauli anayajua haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa wa pili wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yonatani akamwambia: “Usiogope, baba yangu Saulo hatakupata. Wewe utakuwa mufalme wa Israeli, mimi nitakuwa wa pili wako. Hata Saulo baba yangu anajua jambo hili.”