1 Samuel 23:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli na watu wake wakaanza kumtafuta Daudi. Lakini Daudi alipoambiwa habari hizo, alikwenda kujificha kwenye miamba, iliyoko katika mbuga za Maoni na kukaa huko. Shauli aliposikia habari hizo, alimfuatilia Daudi huko kwenye mbuga za Maoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli na watu wake wakaanza msako, naye Daudi alipoelezwa hili, akateremka hadi mwambani na kukaa katika Jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hili, akaenda katika Jangwa la Maoni akimfuata Daudi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta. Watu wakamwambia Daudi; basi kwa hiyo akashuka mpaka mwambani, akakaa nyikani pa Maoni. Naye Sauli alipopata habari, alimwinda Daudi nyikani pa Maoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli na watu wake wakaanza kumtafuta Daudi. Lakini Daudi alipoambiwa habari hizo, alikwenda kujificha kwenye miamba, iliyoko katika mbuga za Maoni na kukaa huko. Shauli aliposikia habari hizo, alimfuatilia Daudi huko kwenye mbuga za Maoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli na watu wake wakaanza msako, naye Daudi alipoelezwa hili, akatelemka mpaka mwambani na kukaa katika Jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hili, akaenda katika Jangwa la Maoni akimfuata Daudi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli na watu wake wakaanza msako, naye Daudi alipoelezwa hili, akateremka mpaka mwambani na kukaa katika Jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hili, akaenda katika Jangwa la Maoni akimfuata Daudi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta. Watu wakamwambia Daudi; basi kwa hiyo akashuka mpaka mwambani, akakaa nyikani pa Maoni. Naye Sauli alipopata habari, alimwinda Daudi nyikani pa Maoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli na watu wake wakaanza kumtafuta Daudi. Lakini Daudi alipoambiwa habari hizo, alikwenda kujificha kwenye miamba, iliyoko katika mbuga za Maoni na kukaa huko. Shauli aliposikia habari hizo, alimfuatilia Daudi huko kwenye mbuga za Maoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli alipokwenda na watu wake kumtafuta, watu wakampasha Dawidi habari; ndipo, aliposhuka mwambani, akakaa katika nyika ya Maoni. Sauli aliposikia, akaja upesi kumfuata kule nyikani kwa Maoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta. Watu wakamwambia Daudi; basi kwa hiyo akashuka mpaka mwambani, akakaa nyikani pa Maoni. Naye Sauli alipopata habari, alimwinda Daudi nyikani pa Maoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo na watu wake wakaanza kumutafuta Daudi. Lakini Daudi alipopata habari zile, alikwenda kujificha kwenye mawe makubwa, yanayokuwa katika mbuga za Maoni na kukaa kule. Saulo aliposikia habari zile, alimufuatilia Daudi kule kwenye mbuga za Maoni.