1 Samuel 23:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shauli na watu wake walikuwa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima. Daudi alipokuwa anaharakisha kukimbia, Shauli naye alikuwa anamkaribia kumkamata Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sauli alikuwa akienda upande mmoja wa mlima, naye Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima, wakiharakisha kumkimbia Sauli. Sauli na majeshi yake walipokaribia kumkamata Daudi na watu wake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana kwenda zake kwa hofu ya Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake wakamzunguka Daudi na watu wake ili kuwakamata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shauli na watu wake walikuwa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima. Daudi alipokuwa anaharakisha kukimbia, Shauli naye alikuwa anamkaribia kumkamata Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sauli alikuwa akienda upande mmoja wa mlima, naye Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima, wakiharakisha kumkimbia Sauli. Wakati Sauli na majeshi yake walipokaribia kumkamata Daudi na watu wake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sauli alikuwa akienda upande mmoja wa mlima, naye Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima, wakiharakisha kumkimbia Sauli. Wakati Sauli na majeshi yake walipokaribia kumkamata Daudi na watu wake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana ili amtoroke Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake walikuwa wakiwazingira Daudi na watu wake ili kuwakamata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shauli na watu wake walikuwa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mlima. Daudi alipokuwa anaharakisha kukimbia, Shauli naye alikuwa anamkaribia kumkamata Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauli akashika njia ya upande wa huku wa mlima ule, naye Dawidi na watu wake wakashika njia ya upande wa huko wa mlima uleule, lakini Dawidi akajihimiza kumkimbia Sauli. Hapo, Sauli na watu wake walipomfikia Dawidi na watu wake na kuwazunguka, wawakamate,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauli akaenda upande huu wa mlima, na Daudi na watu wake wakaenda upande huu wa mlima; naye Daudi akafanya haraka sana kwenda zake kwa hofu ya Sauli; kwa sababu Sauli na watu wake wakamzunguka Daudi na watu wake ili kuwakamata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Saulo na watu wake walikuwa upande mumoja wa mulima, na Daudi na watu wake walikuwa upande mwingine wa mulima. Daudi alipokuwa anaharakisha kukimbia, Saulo naye alikuwa anamukaribia kwa kumukamata Daudi.