1 Samuel 24:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu na aamue kati yangu, na wewe. Yeye akulipize kisasi lakini mimi kamwe sitanyosha mkono wangu dhidi yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu na ahukumu kati yangu na wewe. Naye Mwenyezi Mungu alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana atuamue, mimi na wewe, na Bwana anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu na aamue kati yangu, na wewe. Yeye akulipize kisasi lakini mimi kamwe sitanyosha mkono wangu dhidi yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA na ahukumu kati yangu na wewe. Naye BWANA alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana na ahukumu kati yangu na wewe. Naye bwana alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA atuamue, mimi na wewe, na BWANA anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu na aamue kati yangu, na wewe. Yeye akulipize kisasi lakini mimi kamwe sitanyosha mkono wangu dhidi yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana na atuamue, mimi na wewe! Yeye Bwana na anilipizie kwako! Lakini mkono wangu hautakuinukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA atuamue, mimi na wewe, na BWANA anilipizie kisasi changu kwako; lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia, baba yangu, angalia pindo hili la nguo yako katika mikono yangu. Kwa kulikata pindo la nguo yako bila kukuua, unaweza sasa kujua kwa hakika kwamba mimi si mwovu wala mwasi. Mimi sijatenda zambi juu yako ingawa wewe unaniwinda uniue.