1 Samuel 24:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa nimejua ya kwamba hakika utakuwa mfalme wa Israeli, na ufalme wa Israeli utaimarishwa chini yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa, angalia, najua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa nimejua ya kwamba hakika utakuwa mfalme wa Israeli, na ufalme wa Israeli utaimarishwa chini yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa, angalia, ninajua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa nimejua ya kwamba hakika utakuwa mfalme wa Israeli, na ufalme wa Israeli utaimarishwa chini yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa tazama! Ninajua, ya kuwa utapata kuwa mfalme, nao ufalme wa Waisiraeli utashupaa kwa nguvu za mkono wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa, angalia, najua ya kuwa hakika utakuwa mfalme, na ufalme wa Israeli utafanyika imara mkononi mwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu akimukamata adui yake atamwacha aende salama? Kwa lile ulilonitendea, Yawe akupe zawadi njema!