1 Samuel 24:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, Daudi naye akainuka, akatoka pangoni na kumwita Shauli, “Bwana wangu mfalme!” Mfalme Shauli alipoangalia nyuma, Daudi aliinama hadi chini, akamsujudia Shauli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kumsujudia, uso wake ukigusa chini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hata nchi, akamsujudia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, Daudi naye akainuka, akatoka pangoni na kumwita Shauli, “Bwana wangu mfalme!” Mfalme Shauli alipoangalia nyuma, Daudi aliinama hadi chini, akamsujudia Shauli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hadi chini, akamsujudia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, Daudi naye akainuka, akatoka pangoni na kumwita Shauli, “Bwana wangu mfalme!” Mfalme Shauli alipoangalia nyuma, Daudi aliinama hadi chini, akamsujudia Shauli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baadaye Dawidi naye akaondoka, akatoka mle pangoni, akapaza zauti nyuma yake Sauli kwamba: Bwana wangu mfalme! Sauli alipotazama nyuma, Dawidi akamwinamia mara mbili na kumwangukia chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi naye akainuka baadaye, akatoka pangoni, akamwita Sauli, akisema, Bwana wangu, mfalme. Na Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama uso wake hata nchi, akamsujudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maneno hayo, Daudi akawashawishi watu wake wasimuzuru Saulo; aliwakataza wasimushambulie. Kisha Saulo akasimama, akatoka ndani ya pango akaendelea na safari yake.