1 Samuel 25:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Samweli akafa, nao Waisraeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Parani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akatelemka kwenye Jangwa la Maoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Samweli akafa, nao Israeli wote wakakusanyika na kumwombolezea; wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akateremka kwenye Jangwa la Maoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, Samueli alifariki; nao Waisraeli wote wakakusanyika ili kumwombolezea. Wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye nyika za Parani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile Samweli akafa; ndipo, Waisiraeli wote walipokusanyika kumwombolezea na kumzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Dawidi akaondoka, akatelemka kwenda nyikani kwa Parani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Samweli akakufa. Nao Waisraeli wote wakakusanyika kwa kumwomboleza. Wakamuzika kwenye nyumba yake kule Rama. Kisha Daudi akaenda zake kwenye jangwa za Parani.