1 Samuel 25:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulikuwa na mtu mmoja huko mjini Maoni ambaye alikuwa na biashara ya kondoo mjini Karmeli. Huko Karmeli alifuga kondoo wake na kuwakata manyoya. Alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo 3,000 na mbuzi 1,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na makao huko Karmeli, alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa mkuu sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulikuwa na mtu mmoja huko mjini Maoni ambaye alikuwa na biashara ya kondoo mjini Karmeli. Huko Karmeli alifuga kondoo wake na kuwakata manyoya. Alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo 3,000 na mbuzi 1,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na mali huko Karmeli, yeye alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja huko Maoni, aliyekuwa na makao huko Karmeli, alikuwa tajiri sana. Alikuwa na mbuzi elfu moja na kondoo elfu tatu, aliokuwa akiwakata manyoya huko Karmeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa tajiri sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulikuwa na mtu mmoja huko mjini Maoni ambaye alikuwa na biashara ya kondoo mjini Karmeli. Huko Karmeli alifuga kondoo wake na kuwakata manyoya. Alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo 3,000 na mbuzi 1,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kule Maoni kulikuwa na mtu, nako, alikopatia mali, ni Karmeli; mtu huyo alikuwa mkuu kabisa mwenye kondoo 3000 na mbuzi 1000. Naye siku hizo alikuwa huko Karmeli akiwakata kondoo wake manyoya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huko Maoni kulikuwa na mtu mmoja, ambaye alikuwa na mali yake katika Karmeli; naye yule mtu alikuwa mkuu sana, mwenye kondoo elfu tatu na mbuzi elfu; naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo zake huko Karmeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulikuwa mutu mumoja kule katika muji wa Maoni ambaye alikuwa na biashara ya kondoo katika muji wa Karmeli. Kule Karmeli alifuga kondoo wake na kuwakata manyoya. Alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja.