1 Samuel 25:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa bwana wangu, naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, na vile ulivyo hai, kwamba kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekuzuia usilipize kisasi kwa kumwaga damu na kujipatia lawama, waache adui zako na wale wote wanaokutakia mabaya wawe wapumbavu kama Nabali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Basi sasa, bwana wangu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekuzuia kumwaga damu na kulipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe, hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na kama uishivyo, adui zako na wote wanaokusudia kumdhuru bwana wangu wawe kama Nabali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa bwana wangu, naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, na vile ulivyo hai, kwamba kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekuzuia usilipize kisasi kwa kumwaga damu na kujipatia lawama, waache adui zako na wale wote wanaokutakia mabaya wawe wapumbavu kama Nabali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Basi sasa, kwa kuwa BWANA amekuzuia, wewe bwana wangu, kutokumwaga damu na kutolipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe, hakika kama BWANA aishivyo na kama uishivyo, maadui zako na wote wanaokusudia kumdhuru bwana wangu wawe kama Nabali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Basi sasa, kwa kuwa bwana amekuzuia, wewe bwana wangu, kutokumwaga damu na kutolipiza kisasi kwa mikono yako mwenyewe, hakika kama bwana aishivyo na kama uishivyo, maadui zako na wote wanaokusudia kumdhuru bwana wangu wawe kama Nabali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, bwana wangu, aishivyo BWANA, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa BWANA amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa bwana wangu, naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, na vile ulivyo hai, kwamba kwa kuwa Mwenyezi-Mungu amekuzuia usilipize kisasi kwa kumwaga damu na kujipatia lawama, waache adui zako na wale wote wanaokutakia mabaya wawe wapumbavu kama Nabali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa bwana wangu, kwa hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena kwa hivyo, mwenyewe ulivyo mzima, Bwana amekuzuia, usije kumwaga damu, ukijilipiza kwa mkono wako mwenyewe. Sasa wachukivu wako nao wote wanaomtakia bwana wangu mabaya na wawe kama Nabali!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, bwana wangu, aishivyo BWANA, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa BWANA amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa bwana wangu, kama vile Yawe anavyoishi na kama vile unavyoishi, unaona kwamba Yawe amekuzuia kulipiza kisasi kwa kumwanga damu na hivyo upate kuwa na kosa. Uwaache waadui zako na wale wote wanaokutakia mabaya wakuwe wapumbafu kama Nabali.