1 Samuel 25:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kukitokea watu wakikufuatilia na kutaka kuyaangamiza maisha yako, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atayasalimisha maisha yako pamoja na walio hai. Lakini maisha ya adui zako atayatupilia mbali, kama vile mtu atupavyo jiwe kwa kombeo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata ingawa kuna mtu anayekufuatia ili akuue, usiruhusu baya lolote kuonekana kwako siku zote za maisha yako, uhai wa bwana wangu utafungwa salama kwenye furushi la walio hai na Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Lakini uhai wa adui zako utavurumishwa kama vile jiwe kutoka kombeo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kukitokea watu wakikufuatilia na kutaka kuyaangamiza maisha yako, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atayasalimisha maisha yako pamoja na walio hai. Lakini maisha ya adui zako atayatupilia mbali, kama vile mtu atupavyo jiwe kwa kombeo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata ingawa yuko mtu anayekufuatia kuondoa uhai wako, usiruhusu baya lo lote kuonekana kwako siku zote za maisha yako, uhai wa bwana wangu utafungwa salama kwenye furushi la walio hai na BWANA Mungu wako. Lakini uhai wa adui zako atavurumishwa kama vile jiwe kutoka kwenye kombeo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata ingawa yuko mtu anayekufuatia kuuondoa uhai wako, usiruhusu baya lolote kuonekana kwako siku zote za maisha yako, uhai wa bwana wangu utafungwa salama kwenye furushi la walio hai na bwana Mwenyezi Mungu wako. Lakini uhai wa adui zako atavurumishwa kama vile jiwe kutoka kwenye kombeo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi la uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya kombeo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kukitokea watu wakikufuatilia na kutaka kuyaangamiza maisha yako, Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atayasalimisha maisha yako pamoja na walio hai. Lakini maisha ya adui zako atayatupilia mbali, kama vile mtu atupavyo jiwe kwa kombeo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu atakapoondokea akukimbize na kutafuta njia ya kukuua, ndipo, roho ya bwana wangu itakapokuwa imefungwa vema kifungoni kwao wanaoishi kwake Bwana Mungu wako. Lakini roho za wachukivu wako na azitupe, kama kombeo linavyotupa vijiwe, vikitiwa hapo kati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na BWANA, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kukitokea watu wanaokufuatilia na kutaka kuyaangamiza maisha yako, Yawe, Mungu wako, atayalinda maisha yako pamoja na watu wanaokuwa wazima. Lakini atayatupilia mbali maisha ya waadui zako, kama vile mutu anavyotupa jiwe kwa mujeledi.