1 Samuel 25:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu huyo aliitwa Nabali na mkewe aliitwa Abigaili. Abigaili alikuwa mwanamke mwenye akili na mzuri. Lakini Nabali alikuwa mtu wa chuki na duni; tena alikuwa wa ukoo wa Kalebu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jina la mtu huyo lilikuwa Nabali, naye mkewe aliitwa Abigaili. Alikuwa mwanamke mwenye busara na mzuri wa sura, lakini mumewe, aliyekuwa wa ukoo wa Kalebu, alikuwa mwenye hasira na mchoyo katika utendaji wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu huyo aliitwa Nabali na mkewe aliitwa Abigaili. Abigaili alikuwa mwanamke mwenye akili na mzuri. Lakini Nabali alikuwa mtu wa chuki na duni; tena alikuwa wa ukoo wa Kalebu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Jina la mtu huyo aliitwa Nabali na jina la mkewe aliitwa Abigaili. Alikuwa mwanamke mwenye busara na mzuri wa sura, lakini mumewe, ambaye alikuwa wa ukoo wa Kalebu, alikuwa mwenye hasira na mchoyo katika utendaji wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jina la mtu huyo lilikuwa Nabali, naye mkewe aliitwa Abigaili. Alikuwa mwanamke mwenye busara na mzuri wa sura, lakini mumewe, ambaye alikuwa wa ukoo wa Kalebu, alikuwa mwenye hasira na mchoyo katika utendaji wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema na mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa mkosa adabu na mwovu; naye alikuwa wa ukoo wa Kalebu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu huyo aliitwa Nabali na mkewe aliitwa Abigaili. Abigaili alikuwa mwanamke mwenye akili na mzuri. Lakini Nabali alikuwa mtu wa chuki na duni; tena alikuwa wa ukoo wa Kalebu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo mtu jina lake Nabali, naye mkewe jina lake Abigaili; huyu mkewe alikuwa mwenye akili njema na mwenye umbo zuri, lakini yule mume alikuwa mkorofi mwenye matendo mabaya tu, naye ni wa mlango wa Kalebu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jina la mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake; naye alikuwa wa mbari ya Kalebu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yule aliitwa Nabali na muke wake aliitwa Abigaili. Abigaili alikuwa mwanamuke mwenye akili na sura nzuri. Lakini Nabali alikuwa mutu wa chuki na mutenda maovu; tena alikuwa wa ukoo wa Kalebu.