1 Samuel 25:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wewe bwana wangu, hutakuwa na sababu ya kujuta wala kuhukumiwa na dhamiri kutokana na kumwaga damu bila sababu kwa kujilipiza kisasi. Lakini, bwana wangu, Mwenyezi-Mungu atakapokuwa amekutendea wema huo, nakuomba unikumbuke mimi mtumishi wako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bwana wangu hatakuwa na dhamiri inayolemewa na mzigo kwa kumwaga damu kusiko na sababu, au kujilipizia kisasi yeye mwenyewe. Mwenyezi Mungu atakapomletea bwana wangu mafanikio, umkumbuke mtumishi wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wewe bwana wangu, hutakuwa na sababu ya kujuta wala kuhukumiwa na dhamiri kutokana na kumwaga damu bila sababu kwa kujilipiza kisasi. Lakini, bwana wangu, Mwenyezi-Mungu atakapokuwa amekutendea wema huo, nakuomba unikumbuke mimi mtumishi wako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bwana wangu hatakuwa na dhamiri inayolemewa na mzigo kwa kumwaga damu kusiko na sababu, au kujilipizia kisasi yeye mwenyewe. BWANA atakapomletea bwana wangu mafanikio, umkumbuke mtumishi wako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana wangu hatakuwa na dhamiri inayolemewa na mzigo kwa kumwaga damu kusiko na sababu, au kujilipizia kisasi yeye mwenyewe. bwana atakapomletea bwana wangu mafanikio, umkumbuke mtumishi wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hili halitakuwa kikwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wewe bwana wangu, hutakuwa na sababu ya kujuta wala kuhukumiwa na dhamiri kutokana na kumwaga damu bila sababu kwa kujilipiza kisasi. Lakini, bwana wangu, Mwenyezi-Mungu atakapokuwa amekutendea wema huo, nakuomba unikumbuke mimi mtumishi wako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hapo halitakutonesha, halitaukwaza moyo wa bwana wangu hilo la kwamba: ulimwaga damu bure tu, upate kujiponya mwenyewe, wewe bwana wangu. Kwa hiyo mkumbuke kijakazi wako hapo, Bwana atakapomfanyizia mema bwana wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wewe bwana wangu, hautakuwa na sababu ya kujuta wala kuhukumiwa na zamiri kutokana na kumwanga damu bila sababu kwa kujilipiza kisasi. Lakini, Yawe atakapokuwa amekutendea vizuri, ninakuomba, bwana wangu, unikumbuke mimi mujakazi wako.”