1 Samuel 25:39 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, alisema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amemlipiza kisasi Nabali kwa kunitukana, naye Mwenyezi-Mungu ameniepusha mimi mtumishi wake kutenda maovu. Mwenyezi-Mungu amempatiliza Nabali kwa uovu wake.” Kisha Daudi alituma watu ili wamposee Abigaili awe mke wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, ambaye amenitetea dhidi ya Nabali kwa kuwa alinitendea kwa dharau. Amemzuia mtumishi wake asitende mabaya na Mwenyezi Mungu ameuleta ubaya wa Nabali juu ya kichwa chake mwenyewe.” Kisha Daudi akatuma ujumbe kwa Abigaili kumwomba awe mke wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, Daudi alisema, Na ahimidiwe Bwana ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali Bwana amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, alisema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amemlipiza kisasi Nabali kwa kunitukana, naye Mwenyezi-Mungu ameniepusha mimi mtumishi wake kutenda maovu. Mwenyezi-Mungu amempatiliza Nabali kwa uovu wake.” Kisha Daudi alituma watu ili wamposee Abigaili awe mke wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “Ahimidiwe BWANA, ambaye amenitetea shauri langu dhidi ya Nabali kwa kuwa alinitendea kwa dharau. Amemzuia mtumishi wake asitende mabaya na BWANA ameuleta ubaya wa Nabali juu ya kichwa chake mwenyewe.” Kisha Daudi akatuma ujumbe kwa Abigaili kumwomba awe mke wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “Ahimidiwe bwana, ambaye amenitetea shauri langu dhidi ya Nabali kwa kuwa alinitendea kwa dharau. Amemzuia mtumishi wake asitende mabaya na bwana ameuleta ubaya wa Nabali juu ya kichwa chake mwenyewe.” Kisha Daudi akatuma ujumbe kwa Abigaili kumwomba awe mke wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, alisema, Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, alisema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye amemlipiza kisasi Nabali kwa kunitukana, naye Mwenyezi-Mungu ameniepusha mimi mtumishi wake kutenda maovu. Mwenyezi-Mungu amempatiliza Nabali kwa uovu wake.” Kisha Daudi alituma watu ili wamposee Abigaili awe mke wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi aliposikia, ya kuwa Nabali amekufa, akasema: Na atukuzwe Bwana, kwa kuwa amenigombea huo ugomvi wenye soni, Nabali alionipatia, akamzuia mtumishi wake, asifanye mabaya, nayo mabaya ya Nabali Bwana akayarudisha kumjia kichwani pake. Kisha Dawidi akatuma watu kusema na Abigaili, apate kumchukua, awe mkewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliposikia ya kwamba Nabali amekufa, Daudi alisema, Na ahimidiwe BWANA ambaye amenitetea teto la shutumu langu mkononi mwa Nabali, na kumzuia mtumwa wake asitende maovu; tena uovu wake Nabali BWANA amemrudishia juu ya kichwa chake mwenyewe. Kisha Daudi akatuma watu, akamposa Abigaili ili amwoe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, alisema: “Atukuzwe Yawe ambaye amemulipiza kisasi Nabali kwa kunitukana, naye Yawe ameniepusha mimi mutumishi wake kutenda maovu. Yawe amemwazibu Nabali kwa uovu wake.” Kisha Daudi alituma watu kwa kumuchumbilia Abigaili akuwe muke wake.