1 Samuel 25:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimesikia kwamba unawakata manyoya kondoo wako nataka ujue kwamba wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, nasi hatukuwadhuru. Tena muda wote walipokuwa pamoja nasi mjini Karmeli, hawakukosa chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Nasikia kuwa huu ni wakati wa kukata kondoo manyoya. Wafugaji wako walipokuwa pamoja nasi, hatukuwatendea mabaya na wakati wote waliokuwa huko Karmeli hakuna chochote chao kilipotea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimesikia kwamba unawakata manyoya kondoo wako nataka ujue kwamba wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, nasi hatukuwadhuru. Tena muda wote walipokuwa pamoja nasi mjini Karmeli, hawakukosa chochote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Nasikia kuwa huu ni wakati wa kukata kondoo manyoya. Wachunga mifugo wako walipokuwa pamoja nasi, hatukuwatendea mabaya na wakati wote waliokuwa huko Karmeli hakuna cho chote chao kilichopotea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Nasikia kuwa huu ni wakati wa kukata kondoo manyoya. Wachunga mifugo wako walipokuwa pamoja nasi, hatukuwatendea mabaya na wakati wote waliokuwa huko Karmeli hakuna chochote chao kilipotea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo wako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimesikia kwamba unawakata manyoya kondoo wako nataka ujue kwamba wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, nasi hatukuwadhuru. Tena muda wote walipokuwa pamoja nasi mjini Karmeli, hawakukosa chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nimesikia, ya kuwa wanakukatia manyoya ya kondoo wako; basi, hao wachungaji wako walikuwa kwetu sisi, nasi hatukuwafanyizia kibaya cho chote, wala hakikupotea cho chote kwao siku zote, walipokuwa huku Karmeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami sasa nimesikia ya kuwa una watu wanaokata manyoya kondoo zako; haya! Wachungaji wako wamekuwa pamoja nasi, wala hatukuwadhuru, wala hawakukosa kitu wakati wote walipokuwako huko Karmeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimesikia kwamba unawakata kondoo wako manyoya. Ninataka ujue kwamba wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, nasi hatukuwazuru. Tena muda wote walipokuwa pamoja nasi katika muji wa Karmeli, hawakukosa kitu chochote.