1 Samuel 26:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sasa bwana wangu mfalme, usikie maneno ya mtumishi wako. Ikiwa Mwenyezi-Mungu ndiye aliyekuchochea uje dhidi yangu, basi, na apokee tambiko itakayomfanya abadili nia yake. Lakini kama ni watu, basi, Mwenyezi-Mungu na awalaani watu hao kwani wamenifukuza kutoka urithi aliotupa Mwenyezi-Mungu wakisema, ‘Nenda ukaitumikie miungu mingine.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama Mwenyezi Mungu amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za Mwenyezi Mungu! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa Mwenyezi Mungu wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni Bwana aliyekuondokesha juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za Bwana; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa Bwana, wakisema, Enenda, katumikie miungu mingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sasa bwana wangu mfalme, usikie maneno ya mtumishi wako. Ikiwa Mwenyezi-Mungu ndiye aliyekuchochea uje dhidi yangu, basi, na apokee tambiko itakayomfanya abadili nia yake. Lakini kama ni watu, basi, Mwenyezi-Mungu na awalaani watu hao kwani wamenifukuza kutoka urithi aliotupa Mwenyezi-Mungu wakisema, ‘Nenda ukaitumikie miungu mingine.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama BWANA amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za BWANA! Wao sasa wamenifukuza kutoka katika sehemu yangu katika urithi wa BWANA wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama bwana amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za bwana! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa bwana wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sasa bwana wangu mfalme, usikie maneno ya mtumishi wako. Ikiwa Mwenyezi-Mungu ndiye aliyekuchochea uje dhidi yangu, basi, na apokee tambiko itakayomfanya abadili nia yake. Lakini kama ni watu, basi, Mwenyezi-Mungu na awalaani watu hao kwani wamenifukuza kutoka urithi aliotupa Mwenyezi-Mungu wakisema, ‘Nenda ukaitumikie miungu mingine.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa bwana wangu mfalme na ayasikilize maneno ya mtumishi wake! Kama ni Bwana aliyekuhimiza kunijia, na asikie mnuko wa kipaji cha tambiko! Lakini kama ni watu, na wawe wameapizwa mbele ya Bwana! Kwani wamenifukuza, siku hizi nisiandamane nao walio fungu lake Bwana, wakaniambia: Jiendee kutumikia miungu mingine!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuondokesha juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Enenda, katumikie miungu mingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sasa bwana wangu mufalme, usikie maneno ya mutumishi wako. Ikiwa Yawe ndiye aliyekuchochea ukuje kunishambulia, basi, apokee sadaka ambayo itamusukuma kubadilisha mawazo yake. Lakini ikiwa ni watu, basi, Yawe awalaani watu hao maana wamenifukuza kutoka urizi ambao Yawe aliotupa wakisema: ‘Kwenda uitumikie miungu mingine.’