1 Samuel 26:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu humtunza kila mtu kwa uadilifu na uaminifu wake. Leo Mwenyezi-Mungu alikutia mikononi mwangu, lakini mimi sikunyosha mkono wangu dhidi yako kwa kuwa wewe umeteuliwa naye kwa kutiwa mafuta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu humlipa kila mtu kwa ajili ya haki yake na uaminifu wake. Mwenyezi Mungu alikutia katika mikono yangu leo, lakini sikuinua mkono wangu juu ya mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana Bwana amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu humtunza kila mtu kwa uadilifu na uaminifu wake. Leo Mwenyezi-Mungu alikutia mikononi mwangu, lakini mimi sikunyosha mkono wangu dhidi yako kwa kuwa wewe umeteuliwa naye kwa kutiwa mafuta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA humlipa kila mtu kwa ajili ya haki yake na uaminifu wake. BWANA alikutia katika mikono yangu leo, lakini sikuinua mkono wangu juu ya mpakwa mafuta wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana humlipa kila mtu kwa ajili ya haki yake na uaminifu wake. bwana alikutia katika mikono yangu leo, lakini sikuinua mkono wangu juu ya mpakwa mafuta wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA humlipa kila mtu kulingana na haki na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nilikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu humtunza kila mtu kwa uadilifu na uaminifu wake. Leo Mwenyezi-Mungu alikutia mikononi mwangu, lakini mimi sikunyosha mkono wangu dhidi yako kwa kuwa wewe umeteuliwa naye kwa kutiwa mafuta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bwana atamlipa kila mtu yaupasayo wongofu wake na welekevu wake, maana Bwana amekutia leo mkononi mwangu, lakini nikakataa kuukunjua mkono wangu, nimwue aliyepakwa mafuta na Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anamulinda kila mutu kwa haki yake na uaminifu wake. Leo Yawe alikutia katika mikono yangu, lakini mimi sikunyoosha mukono wangu juu ya yule ambaye ni muchaguliwa wa Yawe.