1 Samuel 27:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi hakumwacha mtu yeyote hai awe mwanamume au mwanamke ili aletwe Gathi; alifikiri moyoni: “Wanaweza wakaeleza juu yetu na kusema, ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo ilikuwa desturi yake wakati wote aliishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi hakumwacha mtu yeyote hai awe mwanamume au mwanamke ili aletwe Gathi; alifikiri moyoni: “Wanaweza wakaeleza juu yetu na kusema, ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana Daudi aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo iliyokuwa desturi yake wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi hakumwacha hai mwanaume au mwanamke ili apate kuletwa Gathi, kwa maana Daudi aliwaza, “Wanaweza kujulisha habari zetu na kusema, ‘Hivi ndivyo alivyofanya Daudi.’ ” Hii ndiyo ilikuwa desturi yake wakati wote aliishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi hakumwacha mtu yeyote hai awe mwanamume au mwanamke ili aletwe Gathi; alifikiri moyoni: “Wanaweza wakaeleza juu yetu na kusema, ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika nchi ya Wafilisti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi asipoacha mume wala mke, asimwue, ni kwa kwamba asiwapeleke Gati, wakayasimulia matendo yetu kwamba: Hivi ndivyo, Dawidi alivyovifanya. Hii desturi yake Dawidi akaifuata siku zile zote, alizokaa katika nchi ya Wafilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Daudi hakumhifadhi hai mume wala mke, ili kuwaleta Gathi maana alisema, Wasituchongee kusema, Ndivyo alivyofanya Daudi, tena ndivyo ilivyokuwa desturi yake wakati wote alipokaa katika nchi ya Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi hakumwacha mutu yeyote muzima akuwe mwanaume au mwanamuke kusudi aletwe Gati; alifikiri ndani ya moyo: “Wanaweza kueleza juu yetu na kusema: ‘Daudi alifanya kitendo hiki na kile.’ ” Hivyo ndivyo Daudi alivyozoea kutenda wakati wote alipoishi katika inchi ya Wafilistini.