1 Samuel 27:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali mbele yako nakuomba unipe mji mmoja nchini mwako ili uwe mahali pangu pa kuishi. Hakuna haja kwangu kuishi nawe katika mji huu wa kifalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, unipe sehemu katika mojawapo ya miji katika nchi nikae huko. Kwa nini mtumwa wako akae pamoja nawe katika mji huu wa kifalme?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali mbele yako nakuomba unipe mji mmoja nchini mwako ili uwe mahali pangu pa kuishi. Hakuna haja kwangu kuishi nawe katika mji huu wa kifalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, unipe sehemu katika mojawapo ya miji katika nchi nikae huko, kwa nini mtumwa wako akae pamoja nawe katika mji huu wa kifalme?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, unipe sehemu katika mojawapo ya miji katika nchi nikae huko. Kwa nini mtumwa wako akae pamoja nawe katika mji huu wa kifalme?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumishi wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali mbele yako nakuomba unipe mji mmoja nchini mwako ili uwe mahali pangu pa kuishi. Hakuna haja kwangu kuishi nawe katika mji huu wa kifalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akamwambia Akisi: Kama nimeona upendeleo machoni pako, na wanipe pa kukaa katika mji mmoja wa porini, nikae huko! Inakuwaje, mtumishi wako akikaa kwako katika mji wa kifalme?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona kibali machoni pako na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja, Daudi akamwambia Akisi: “Kama nimepata kukubaliwa mbele yako, ninakuomba unipe muji mumoja katika inchi yako kusudi ukuwe pahali pangu pa kuishi. Hakuna faida kwangu kuishi nawe katika muji huu wa kifalme.”