1 Samuel 27:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika muda huo, Daudi na watu wake waliwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki, ambao walikuwa wenyeji wa nchi hiyo tangu zamani. Aliwashambulia katika nchi yao mpaka Shuri, mpakani na Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika muda huo, Daudi na watu wake waliwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki, ambao walikuwa wenyeji wa nchi hiyo tangu zamani. Aliwashambulia katika nchi yao mpaka Shuri, mpakani na Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia itelemkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Daudi na watu wake wakapanda na kuwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki. (Tangu zamani haya mataifa yalikuwa yameishi kwenye eneo lililotanda kuanzia Telemu katika njia iteremkayo Shuri hadi kufikia nchi ya Misri.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, mpaka nchi ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika muda huo, Daudi na watu wake waliwashambulia Wageshuri, Wagirizi na Waamaleki, ambao walikuwa wenyeji wa nchi hiyo tangu zamani. Aliwashambulia katika nchi yao mpaka Shuri, mpakani na Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Dawidi na watu wake walipopanda, wakawashambulia Wagesuri na Wagirzi na Waamaleki, kwani hawa ndio waliokaa katika nchi hiyo tangu zamani zote, kufika Suri hata nchi ya Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, hata mpaka nchi ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika muda huo, Daudi na watu wake waliwashambulia Wagesuri, Wagirzi na Waamaleki, ambao walikuwa wenyeji wa inchi hiyo tangu zamani. Aliwashambulia katika inchi yao mpaka Suri, hata kwa mupaka na Misri.