1 Samuel 27:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi aliipiga nchi hiyo asimwache hai mtu yeyote, awe mwanamume au mwanamke, akateka kondoo, ng'ombe, punda, ngamia na mavazi; kisha akarudi na kufika kwa Akishi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mara Daudi aliposhambulia eneo, hakubakiza hai mwanaume wala mwanamke, lakini alichukua kondoo na ng’ombe, punda na ngamia, na nguo. Kisha akarudi kwa Akishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng'ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi aliipiga nchi hiyo asimwache hai mtu yeyote, awe mwanamume au mwanamke, akateka kondoo, ng'ombe, punda, ngamia na mavazi; kisha akarudi na kufika kwa Akishi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mara Daudi aliposhambulia eneo, hakubakiza hai mwanaume wala mwanamke, lakini alichukua kondoo na ng'ombe, punda na ngamia, na nguo. Kisha akarudi kwa Akishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mara Daudi aliposhambulia eneo, hakubakiza hai mwanaume wala mwanamke, lakini alichukua kondoo na ng’ombe, punda na ngamia, na nguo. Kisha akarudi kwa Akishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng'ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi aliipiga nchi hiyo asimwache hai mtu yeyote, awe mwanamume au mwanamke, akateka kondoo, ng'ombe, punda, ngamia na mavazi; kisha akarudi na kufika kwa Akishi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi alipoipiga hiyo nchi, hakuacha mume wala mke, asimwue, akachukua mbuzi na kondoo na ng'ombe na punda na ngamia na nguo, kisha akarudi kufika kwa Akisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Daudi akaipiga nchi hiyo, asimhifadhi hai mume wala mke, akateka nyara kondoo, na ng’ombe, na punda, na ngamia na mavazi; kisha akarejea na kufika kwa Akishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi aliipiga inchi hiyo pasipo kuacha mutu yeyote muzima, akuwe mwanaume au mwanamuke, akateka kondoo, ngombe, punda, ngamia na nguo; kisha akarudi na kufika kwa Akisi.