1 Samuel 28:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ghafla, Shauli akiwa na hofu kutokana na maneno ya Samueli, alianguka kifudifudi; hakuwa na nguvu zozote; kwa kuwa alikuwa hajala chochote kwa siku nzima, usiku na mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Papo hapo Sauli akaanguka chini, akajinyoosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala chochote mchana ule wote na usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ghafla, Shauli akiwa na hofu kutokana na maneno ya Samueli, alianguka kifudifudi; hakuwa na nguvu zozote; kwa kuwa alikuwa hajala chochote kwa siku nzima, usiku na mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Papo hapo Sauli akaanguka chini, akajinyosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala cho chote mchana ule wote na usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Papo hapo Sauli akaanguka chini, akajinyoosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala chochote mchana ule wote na usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara Sauli akaanguka chini kifudifudi, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yoyote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ghafla, Shauli akiwa na hofu kutokana na maneno ya Samueli, alianguka kifudifudi; hakuwa na nguvu zozote; kwa kuwa alikuwa hajala chochote kwa siku nzima, usiku na mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo Sauli akaanguka chini kifudifudi, akashikwa na woga kabisa kwa ajili ya maneno ya Samweli, hata nguvu haikuwamo mwake, kwani alikuwa hakula chakula mchana kutwa na usiku kucha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa rafla, Saulo akiwa na hofu kutokana na maneno ya Samweli, alianguka chini. Hakukuwa na nguvu zozote kwa sababu alikuwa hajakula kitu chochote kwa siku nzima, usiku na muchana.