1 Samuel 29:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakuu watano wa Wafilisti walipokuwa wakipita na vikosi vyao vya mamia na maelfu, Daudi naye akiwa na watu wake pamoja na Akishi walikuwa wanafuata upande wa nyuma wa jeshi hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakuu watano wa Wafilisti walipokuwa wakipita na vikosi vyao vya mamia na maelfu, Daudi naye akiwa na watu wake pamoja na Akishi walikuwa wanafuata upande wa nyuma wa jeshi hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakuu wa Wafilisti wakapita mbele, mamia, na maelfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakuu watano wa Wafilisti walipokuwa wakipita na vikosi vyao vya mamia na maelfu, Daudi naye akiwa na watu wake pamoja na Akishi walikuwa wanafuata upande wa nyuma wa jeshi hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wakuu wa Wafilisti wakafika hapo kuyapanga mamia na maelfu yao; naye Dawidi akafika na watu wake kuwapanga nyuma ya Akisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa watano wa Wafilistini walipokuwa wakipita na makundi yao ya waaskari ya mamia na maelfu, Daudi naye akiwa na watu wake pamoja na Akisi walikuwa wanafuata upande wa nyuma wa kundi lile.