1 Samuel 29:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kwamba umekuwa mwaminifu kwangu. Lingekuwa jambo jema kwangu twende wote vitani, kwa maana sijaona lolote baya kwako tangu siku ile ulipokuja kwangu hadi leo hii. Hata hivyo, wakuu hawajaridhika nawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lolote kwako, lakini hao watawala hawakukubali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo Bwana, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kwamba umekuwa mwaminifu kwangu. Lingekuwa jambo jema kwangu twende wote vitani, kwa maana sijaona lolote baya kwako tangu siku ile ulipokuja kwangu hadi leo hii. Hata hivyo, wakuu hawajaridhika nawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Kama vile BWANA aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lo lote kwako, lakini hao watawala hawakukubali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Kama vile bwana aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lolote kwako, lakini hao watawala hawakukubali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo BWANA, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai, kwamba umekuwa mwaminifu kwangu. Lingekuwa jambo jema kwangu twende wote vitani, kwa maana sijaona lolote baya kwako tangu siku ile ulipokuja kwangu hadi leo hii. Hata hivyo, wakuu hawajaridhika nawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Akisi alipomwita Dawidi, akamwambia: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, wewe u mtu mnyofu! Kwa hiyo ilifaa machoni pangu, utoke pamoja nami, uingie katika vita hivi pamoja nami, kwani sikuona kwako kibaya cho chote tangu siku hiyo, ulipokuja kwangu, hata siku hii ya leo; lakini machoni pao wakuu wewe hufai.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Akishi akamwita Daudi, akamwambia, Aishivyo BWANA, wewe umekuwa mwenye adili, tena kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema machoni pangu; kwa sababu mimi sikuona uovu ndani yako tangu siku ile uliponijia hata leo; walakini hao wakuu hawakuridhii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akisi akamwita Daudi na kumwambia: “Kama vile Yawe anavyoishi, umekuwa mutu wa usawa. Ingekuwa jambo zuri kwangu tuende wote katika vita, kwa maana sijaona jambo baya lolote kwako tangu siku ile ulipokuja kwangu mpaka leo hii. Hata hivyo, wakubwa hawajapendezwa nawe.