1 Samuel 30:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa watu mia mbili walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu mia nne wakaendelea kufuatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Daudi akaendelea kuwafuatilia, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile genge akiwa na watu 400, watu 200 wakabaki hapo kwani walichoka mno, wasiweze kuvuka kijito hicho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Dawidi na watu 400 wakaendelea kupiga mbio, waliokaa ni 200 tu, ndio wale waliochoka sana, wasiweze kuvuka mtoni kwa Besori.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Daudi aliendelea kulifuatilia lile kundi akiwa na watu mia ine. Watu mia mbili wakabaki pale kwa sababu walichoka sana hata hawakuweza kuvuka kijito kile.