1 Samuel 30:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwuliza, “Bwana wako ni nani? Na umetoka wapi?” Yeye akamwambia, “Mimi ni kijana Mmisri. Ni mtumishi wa Mmaleki mmoja. Bwana wangu aliniacha nyuma siku tatu zilizopita kwa kuwa nilikuwa mgonjwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?” Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani; nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na ugonjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwuliza, “Bwana wako ni nani? Na umetoka wapi?” Yeye akamwambia, “Mimi ni kijana Mmisri. Ni mtumishi wa Mmaleki mmoja. Bwana wangu aliniacha nyuma siku tatu zilizopita kwa kuwa nilikuwa mgonjwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?” Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?” Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe ni mtu wa nani; na umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nilishikwa na ugonjwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwuliza, “Bwana wako ni nani? Na umetoka wapi?” Yeye akamwambia, “Mimi ni kijana Mmisri. Ni mtumishi wa Mmaleki mmoja. Bwana wangu aliniacha nyuma siku tatu zilizopita kwa kuwa nilikuwa mgonjwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Dawidi alipomwuliza: Wewe mtu wa nani? Unatoka wapi? Akasema: Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa mtu wa Amaleki; bwana wangu akaniacha, kwa kuwa naliugua, leo ni siku ya tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani; nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na ugonjwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwuliza: “Bwana wako ni nani? Na umetoka wapi?” Yeye akamwambia: “Mimi ni kijana Mumisri. Ni mutumishi wa Mwamaleki mumoja. Bwana wangu aliniacha nyuma siku tatu zilizopita kwa maana nilikuwa mugonjwa.