1 Samuel 30:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule kijana alimwongoza Daudi hadi genge lile lilipokuwa. Walipofika huko waliwakuta wateka nyara hao wakiwa wametawanyika kila mahali kwani walikuwa wakila na kunywa kwa sababu nyara walizoteka kutoka nchi ya Wafilisti na nchi ya Yuda zilikuwa nyingi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwongoza Daudi hadi mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule kijana alimwongoza Daudi hadi genge lile lilipokuwa. Walipofika huko waliwakuta wateka nyara hao wakiwa wametawanyika kila mahali kwani walikuwa wakila na kunywa kwa sababu nyara walizoteka kutoka nchi ya Wafilisti na nchi ya Yuda zilikuwa nyingi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka katika nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule kijana alimwongoza Daudi hadi genge lile lilipokuwa. Walipofika huko waliwakuta wateka nyara hao wakiwa wametawanyika kila mahali kwani walikuwa wakila na kunywa kwa sababu nyara walizoteka kutoka nchi ya Wafilisti na nchi ya Yuda zilikuwa nyingi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawaongoza, wakawakuta; nao walikuwa wametawanyika katika nchi hiyo yote, wakawa wanakula, wanakunywa, maana walikula sikukuu kwa ajili ya hayo mateka yote yaliyokuwa makubwa, waliyoyateka katika nchi ya Wafilisti na katika nchi ya Yuda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule kijana alimwongoza Daudi mpaka kwenye kundi lile. Walipofika kule waliwakuta wanyanganyi wale wakiwa wametawanyika kila pahali maana walikuwa wakikula na kunywa kwa sababu vitu walivyonyanganya kutoka inchi ya Wafilistini na inchi ya Yuda vilikuwa vingi sana.