1 Samuel 30:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akawaambia, “Sivyo ndugu zangu. Hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Mwenyezi-Mungu ametupa. Alitulinda salama, na akalitia mikononi mwetu genge lililokuja kutushambulia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akajibu, “La, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Mwenyezi Mungu ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa Bwana, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akawaambia, “Sivyo ndugu zangu. Hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Mwenyezi-Mungu ametupa. Alitulinda salama, na akalitia mikononi mwetu genge lililokuja kutushambulia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho BWANA ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa BWANA, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akawaambia, “Sivyo ndugu zangu. Hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Mwenyezi-Mungu ametupa. Alitulinda salama, na akalitia mikononi mwetu genge lililokuja kutushambulia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini Dawidi akasema: Msifanye hivyo, ndugu zangu, kuyatumia hivyo, Bwana aliyotupa! Naye ametulinda, akakitia kile kikosi kilichotujia mikononi mwetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa BWANA, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akawaambia: “Sivyo wandugu zangu. Hamuwezi kufanya vile kwa kile ambacho Yawe ametupatia. Alitulinda salama, na akalitia katika mikono yetu kundi lililokuja kutushambulia.