1 Samuel 30:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi na watu wake walipofika mjini waliukuta mji umeteketezwa, na wanawake, watoto wao wa kiume na wa kike, wamechukuliwa mateka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao wa kiume na wa kike wamechukuliwa mateka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi na watu wake walipofika mjini waliukuta mji umeteketezwa, na wanawake, watoto wao wa kiume na wa kike, wamechukuliwa mateka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi na watu wake walipoufikia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, wanaume kwa wanawake, wamechukuliwa mateka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi na watu wake walipofika mjini waliukuta mji umeteketezwa, na wanawake, watoto wao wa kiume na wa kike, wamechukuliwa mateka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi na watu wake walipofika mjini, wakauona mji kuwa umeteketezwa kwa moto, nao wake zao na watoto wao wa kiume na wa kike walikuwa wametekwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi na watu wake walipofika katika muji waliukuta muji umeteketezwa, na wanawake, watoto wao wanaume na wanawake wamekamatwa mateka.