1 Samuel 30:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, Daudi alikuwa katika matatizo makubwa kwa kuwa watu wake walikuwa na uchungu rohoni mwao kwa kupoteza watoto wao; hivyo wakawa wanamtishia kumpiga mawe. Lakini Daudi alijipa moyo kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana kuhusu kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe wa kiume na wa kike. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, Daudi alikuwa katika matatizo makubwa kwa kuwa watu wake walikuwa na uchungu rohoni mwao kwa kupoteza watoto wao; hivyo wakawa wanamtishia kumpiga mawe. Lakini Daudi alijipa moyo kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika bwana, Mungu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, Daudi alikuwa katika matatizo makubwa kwa kuwa watu wake walikuwa na uchungu rohoni mwao kwa kupoteza watoto wao; hivyo wakawa wanamtishia kumpiga mawe. Lakini Daudi alijipa moyo kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akasongeka sana, kwani wale watu walitaka kumpiga mawe, kwa kuwa wote pia walikuwa na uchungu rohoni, kila mmoja kwa ajili ya watoto wake wa kiume na wa kike. Ndipo, Dawidi alipojipatia nguvu kwa Bwana Mungu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, Daudi alikuwa katika matatizo makubwa kwa sababu watu wake walikuwa na uchungu katika roho zao kwa kupoteza watoto wao. Kwa hiyo wakakuwa wakitaka kumupiga mawe. Lakini Daudi alijipa moyo kwa kumutegemea Yawe, Mungu wake.