1 Samuel 30:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, genge hili nilifuate? Na je nitalikamata?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Lifuate kwani utalipata na kuwaokoa hao waliotekwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye Daudi akamuuliza Mwenyezi Mungu, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?” Mwenyezi Mungu akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, genge hili nilifuate? Na je nitalikamata?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Lifuate kwani utalipata na kuwaokoa hao waliotekwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye Daudi akamwuliza BWANA, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?” BWANA akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye Daudi akamuuliza bwana, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?” bwana akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwomba Mwenyezi-Mungu shauri, “Je, genge hili nilifuate? Na je nitalikamata?” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Lifuate kwani utalipata na kuwaokoa hao waliotekwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akamwuliza Bwana kwamba: Nikikimbia na kukifuata hicho kikosi nitakipata? Akamwambia: Piga mbio! Kwani utakipata kweli, uwaponye mateka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akauliza kwa BWANA, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwomba Yawe shauri: “Nikifuata kundi hili nitalikamata?” Yawe akamujibu: “Ulifuate maana utalipata na kuwaokoa hao waliotekwa.”