1 Samuel 30:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi pamoja na watu wake mia sita wakafika kwenye Bonde la Besori, ambapo wengine waliachwa nyuma,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu 600 aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta baadhi ya watu waliotekwa wameachwa hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Dawidi alipokwenda yeye na wale watu 600 waliokuwa naye, wakafika mtoni kwa Besori; huko ndiko, walikokaa wao walioachwa nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Daudi akaondoka pamoja na wale watu mia sita aliokuwa nao. Walipofika kwenye kijito cha Besori, wakawakuta wamoja kati ya watu waliotekwa wameachwa pale.