1 Samuel 31:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao Waisraeli waliokuwa upande wa pili wa bonde, na wengine waliokuwa upande wa mashariki wa mto Yordani walipoona kuwa Waisraeli wamekimbia, naye Shauli na wanawe wamekufa, waliihama miji yao, wakakimbia. Wafilisti wakaenda na kukaa katika miji hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waisraeli waliokuwa kando ya bonde na wale waliokuwa ng’ambo ya Yordani walipoona kuwa jeshi la Waisraeli limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaacha miji yao na kukimbia. Nao Wafilisti wakaenda na kukaa humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao Waisraeli waliokuwa upande wa pili wa bonde, na wengine waliokuwa upande wa mashariki wa mto Yordani walipoona kuwa Waisraeli wamekimbia, naye Shauli na wanawe wamekufa, waliihama miji yao, wakakimbia. Wafilisti wakaenda na kukaa katika miji hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waisraeli waliokuwa kandokando ya bonde na wale waliokuwa ng'ambo ya Yordani walipoona kuwa jeshi la Waisraeli limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaacha miji yao na kukimbia. Nao Wafilisti wakaja na kumiliki humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waisraeli waliokuwa kandokando ya bonde na wale waliokuwa ng’ambo ya Yordani walipoona kuwa jeshi la Waisraeli limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, wakaacha miji yao na kukimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao Waisraeli waliokuwa upande wa pili wa bonde, na wengine waliokuwa upande wa mashariki wa mto Yordani walipoona kuwa Waisraeli wamekimbia, naye Shauli na wanawe wamekufa, waliihama miji yao, wakakimbia. Wafilisti wakaenda na kukaa katika miji hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wa Waisiraeli waliokaa ng'ambo ya huko ya hilo bonde na ng'ambo ya huko ya Yordani walipoona, ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia nao; kisha Wafilisti wakaja, wakakaa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng’ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao Waisraeli waliokuwa upande wa pili wa bonde, na wengine waliokuwa upande wa mashariki wa muto Yordani walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, naye Saulo na wana wake wamekufa, waliihama miji yao, wakakimbia. Wafilistini wakaenda na kukaa katika miji hiyo.