1 Samuel 4:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wafilisti walipiga vita, na Waisraeli walishindwa na kukimbia kila mtu nyumbani kwake. Siku hiyo kulikuwa na mauaji makubwa kwani askari wa miguu 30,000 wa Israeli waliuawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Wafilisti wakapigana, nao Waisraeli wakashindwa na kila mtu akakimbilia kwenye hema lake. Mauaji yalikuwa makubwa sana, Israeli wakapoteza askari elfu thelathini walioenda kwa miguu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wafilisti walipiga vita, na Waisraeli walishindwa na kukimbia kila mtu nyumbani kwake. Siku hiyo kulikuwa na mauaji makubwa kwani askari wa miguu 30,000 wa Israeli waliuawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Wafilisti wakapigana, nao Waisraeli wakashindwa na kila mtu akakimbilia hemani mwake. Mauaji yalikuwa makubwa sana, Israeli wakapoteza askari 30,000 waendao kwa miguu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Wafilisti wakapigana, nao Waisraeli wakashindwa na kila mtu akakimbilia hemani mwake. Mauaji yalikuwa makubwa sana, Israeli wakapoteza askari 30,000 waendao kwa miguu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu elfu thelathini walioenda vitani kwa miguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wafilisti walipiga vita, na Waisraeli walishindwa na kukimbia kila mtu nyumbani kwake. Siku hiyo kulikuwa na mauaji makubwa kwani askari wa miguu 30,000 wa Israeli waliuawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Wafilisti walipopigana nao, Waisiraeli wakapigwa, wakakimbilia kwao kila mtu hemani kwake; likawa pigo kubwa sana, kwao Waisiraeli wakauawa 30000 waliokwenda kwa miguu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu thelathini elfu wenye kwenda vitani kwa miguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wafilistini walipiga vita, na Waisraeli walishindwa na kukimbia kila mutu kwake. Siku hiyo kulikuwa mauaji makubwa maana waaskari wa miguu elfu makumi tatu wa Israeli waliuawa.