1 Samuel 4:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Eli, akiwa na wasiwasi moyoni kuhusu sanduku la Mungu, alikuwa ameketi kwenye kiti chake, kando ya barabara akiangalia. Yule mtu alipowasili mjini na kueleza habari hizo, mji mzima ulilia kwa sauti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipofika, Eli alikuwa ameketi kwenye kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kueleza kilichokuwa kimetokea, mji wote ukalia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Eli, akiwa na wasiwasi moyoni kuhusu sanduku la Mungu, alikuwa ameketi kwenye kiti chake, kando ya barabara akiangalia. Yule mtu alipowasili mjini na kueleza habari hizo, mji mzima ulilia kwa sauti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipofika, Eli alikuwa ameketi juu ya kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kueleza ni nini kilichokuwa kimetokea, mji wote ukalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipofika, Eli alikuwa ameketi juu ya kiti chake kando ya barabara akiangalia, kwa sababu moyo wake ulikuwa na hofu kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kueleza kilichokuwa kimetokea, mji wote ukalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Eli, akiwa na wasiwasi moyoni kuhusu sanduku la Mungu, alikuwa ameketi kwenye kiti chake, kando ya barabara akiangalia. Yule mtu alipowasili mjini na kueleza habari hizo, mji mzima ulilia kwa sauti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika akamwona Eli, akikaa langoni katika kiti chake cha ukuu kando ya njia na kuchungulia njiani, kwani moyo wake ulikuwa umehangaika kwa ajili ya Sanduku la Mungu. Yule mtu alipoingia mjini kupasha habari, watu wote wa mjini wakalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea; maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Eli, akiwa na wasiwasi ndani ya moyo juu ya Sanduku la Mungu, alikuwa ameikaa kwenye kiti chake, pembeni ya barabara akiangalia. Yule mutu alipofika katika muji na kueleza habari hizo, muji muzima ulilia kwa sauti.