1 Samuel 4:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtu akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi; nimekimbia kutoka vitani leo.” Eli akamwuliza, “Mwanangu, mambo yalikuwaje huko?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka huko siku ya leo.” Eli akamuuliza, “Je, mwanangu, ni nini kimetokea huko?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtu akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi; nimekimbia kutoka vitani leo.” Eli akamwuliza, “Mwanangu, mambo yalikuwaje huko?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka huko leo hii.” Eli akamwuliza, “Je, mwanangu, ni nini kimetokea huko?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi, nimekimbia kutoka huko leo hii.” Eli akamuuliza, “Je, mwanangu, ni nini kimetokea huko?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtu akamwambia Eli, “Mimi nimetoka vitani sasa hivi; nimekimbia kutoka vitani leo.” Eli akamwuliza, “Mwanangu, mambo yalikuwaje huko?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu akamwambia Eli: Mimi nimetoka hapo, walipojipanga kupigana; nami nimekimbia leo hivi kutoka hapo, walipojipanga kupigana. Akauliza: Mambo ya huko yako namna gani, mwanangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema, Yalikwendaje, mwanangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutu akamwambia Eli: “Mimi nimetoka kwenye vita; nimekimbia kutoka katika vita leo.” Eli akamwuliza: “Mwana wangu, mambo yalikuwa namna gani kule?”