1 Samuel 4:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule aliyeleta habari akasema, “Waisraeli wamewakimbia Wafilisti. Kumekuwa na mauaji makubwa miongoni mwa Waisraeli. Zaidi ya yote, wanao wote wawili, Hofni na Finehasi, wameuawa, na sanduku la agano la Mungu limetekwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mtu aliyeleta habari akajibu, “Waisraeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, na wanajeshi wengi sana wameuawa. Pia wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa, na Sanduku la Mungu limetekwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule aliyeleta habari akasema, “Waisraeli wamewakimbia Wafilisti. Kumekuwa na mauaji makubwa miongoni mwa Waisraeli. Zaidi ya yote, wanao wote wawili, Hofni na Finehasi, wameuawa, na sanduku la agano la Mungu limetekwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mtu aliyeleta habari akajibu, “Israeli amekimbia mbele ya Wafilisti, nalo jeshi limepata hasara kubwa. Pia wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa, na Sanduku la Mungu limetekwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mtu aliyeleta habari akajibu, “Israeli amekimbia mbele ya Wafilisti, nalo jeshi limepata hasara kubwa. Pia wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa, na Sanduku la Mungu limetekwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule aliyeleta habari akasema, “Waisraeli wamewakimbia Wafilisti. Kumekuwa na mauaji makubwa miongoni mwa Waisraeli. Zaidi ya yote, wanao wote wawili, Hofni na Finehasi, wameuawa, na sanduku la agano la Mungu limetekwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye kuleta habari akajibu na kusema: Waisiraeli wamekimbizwa na Wafilisti, likawa pigo kubwa sana kwao, nao wanao wawili, Hofuni na Pinehasi, wamekufa, hata Sanduku la Mungu limetekwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule aliyeleta habari akasema: “Waisraeli wamewakimbia Wafilistini. Kumekuwa mauaji makubwa kati ya Waisraeli. Zaidi ya yote, wana wako wote wawili, Hofuni na Finehasi, wameuawa, na Sanduku la Agano la Mungu limetekwa.”